Nov 4, 2022
Hoja na tafakuri ulizozichambua hapa ni muhimu kwa jamii zetu na nitajitahidi nikisome kitabu hiki. Swali kuu lililonigusa kama mwanadiaspora na pia mzaliwa wa Tanzania mwenye jina la kigeni, ni swali la mtanzania ni nani? Imenikumbusha machungu niliyoyapitia binafsi nikiwa nyumbani na ughaibuni...