Member-only story
Je, Wewe Ni Mbaguzi?
Shairi lisilo na vina wala mizani
Jun 5, 2020
Unapofikiria yeye ni:
mshamba
wa kuja
wa mjini
wa kijiweni
mvutaji
tajiri
maskini.
Unaposema yeye hana:
mtindi
mwili
wowo
unywele.
Unaposema yeye ana:
ubapa
mianzi
tege
njiti
kipilipili.
Unapomuita yeye ni:
bundi
jalala
cheupe
cheusi
shombe
mhindi koko
mzungu pori.
Je, wewe ni mbaguzi?
Author’s note:
* This poem, intentionally in my mother tongue Kiswahili, pauses a question if one is discriminatory based on the phrases and nicknames used in our everyday Swahili language.